You are currently viewing MKUTANO MKUU WA CHAMA WA SABA MWAKA 2025

MKUTANO MKUU WA CHAMA WA SABA MWAKA 2025

Mkutano Mkuu wa Saba wa Chama Kikuu cha Ushirika Milambo

Mkutano Mkuu wa Saba wa Chama Kikuu cha Ushirika MILAMBO ulifanyika tarehe 30/04/2025 na kuhudhuriwa na Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Paul Matiko Chacha. Katika hotuba yake, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliwasisitiza wanachama kuimarisha mshikamano, kuongeza uwajibikaji na kushirikiana kwa dhati ili kuhakikisha chama kinaendelea kuwa nguzo ya maendeleo ya kilimo na uchumi wa wakulima.

Mkutano huu uliwakutanisha wajumbe kutoka vyama vya msingi vinavyounda chama na ni sehemu muhimu ya uendeshaji wa ushirika, kwani hutoa fursa kwa wanachama kujadili maendeleo, changamoto na mikakati ya kuinua shughuli za chama.

Mambo makuu yaliyojadiliwa ni pamoja na:

  • Taarifa za utekelezaji wa shughuli za chama kwa mwaka uliopita.
  • Mapato na matumizi ya chama.
  • Mafanikio yaliyopatikana katika kusambaza pembejeo na masoko ya mazao ya wanachama.
  • Kupitisha maazimio mapya kwa ajili ya kuboresha huduma kwa wanachama.

Leave a Reply