MRAJIS TAIFA ATEMBELEA BANDA LA MILAMBO KATIKA MAONYESHO YA NANENANE
Katika kuendelea kutambua mchango wa vyama vya ushirika katika maendeleo ya kilimo na ustawi wa wakulima nchini, Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Dr. Benson Ndiege alitembelea banda la Chama Kikuu cha Ushirika MILAMBO (MILAMBO CU LTD) katika Maonyesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani Dodoma.
Katika ziara hiyo, Mrajis alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na MILAMBO, zikiwemo usambazaji wa pembejeo bora kwa wakulima wa tumbaku, huduma za ugani, uwekezaji wa kiuchumi kwa wakulima kupitia vyama vya msingi (AMCOS), pamoja na juhudi za kutafuta masoko ya uhakika kwa mazao ya wanachama.
#Nanenane2025
#MilamboCU
#KilimoNiBiashara