You are currently viewing MAFUNZO KWA MAKATIBU/WAHASIBU WA VYAMA VYA MSINGI(AMCOS) WILAYANI KALIUA NA URAMBO

MAFUNZO KWA MAKATIBU/WAHASIBU WA VYAMA VYA MSINGI(AMCOS) WILAYANI KALIUA NA URAMBO

Mafunzo kwa Makatibu/Wahasibu Kuhusu Utaratibu Mpya wa Utoaji wa Ankara, Makisio na Mali Kupitia Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU)

Ofisi ya Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Tabora iliandaa mafunzo maalum kwa makatibu wa vyama vya ushirika kutoka wilaya za Urambo na Kaliua kuhusu utaratibu mpya wa utoaji wa ankara za malipo, makisio na mali kupitia mfumo wa usimamizi wa vyama vya ushirika (MUVU).

Mafunzo hayo yalifanyika kuanzia tarehe 11.08.2025 hadi tarehe 12.08.2025, yakiongozwa na Afisa TEHAMA kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Ndugu Daudi Mohamed, kwa kushirikiana na Afisa TEHAMA wa Chama Kikuu cha Ushirika Milambo.

Kupitia mafunzo haya, makatibu waliweza kupata uelewa wa kina juu ya matumizi ya mfumo wa MUVU katika kusimamia shughuli za kifedha na mali za vyama vyao, ikiwemo uandaaji na utoaji sahihi wa ankara, makisio na taarifa za mali. Hatua hii inalenga kuongeza uwazi, ufanisi na uwajibikaji katika uendeshaji wa vyama vya ushirika.

Leave a Reply