Ziara ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Ndg. Samuel Mshote katika Ofisi za Chama Kikuu cha Ushirika MILAMBO
Chama Kikuu cha Ushirika MILAMBO CU LTD kimepata heshima ya kutembelewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), Ndg. Samuel Mshote.
Lengo kuu la ziara hii lilikuwa kujadiliana na uongozi wa chama kuhusu masuala ya upatikanaji wa mbolea kwa wakati na usambazaji wake kwa vyama vya msingi (AMCOS) vilivyo chini ya MILAMBO.
Uongozi wa MILAMBO CU LTD umeishukuru TFC kwa kuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya sekta ya kilimo kupitia ushirika.