Mkutano muhimu wa watendaji wa Vyama vya Msingi (AMCOS) kutoka Wilaya ya Urambo na Kaliua umefanyika kwa lengo la kuimarisha utendaji, kuongeza uwajibikaji, na kujenga uelewa wa pamoja juu ya maboresho katika usimamizi wa shughuli za vyama. Washiriki wa mkutano huu walijumuisha makatibu meneja na wahasibu wa AMCOS, pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ya kilimo cha tumbaku na ushirika.
Mkutano ulihitimishwa kwa maazimio kadhaa ambayo yanalenga kuimarisha utendaji wa vyama, kuongeza nidhamu ya kiutawala, na kuhakikisha AMCOS zinaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya kilimo na uchumi katika wilaya hizi mbili.





