Wajumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika MILAMBO wamefanya ziara maalum katika vyama wanachama kwa lengo la kusikiliza kero, maoni na mapendekezo ya wakulima. Ziara hiyo imelenga kuimarisha mawasiliano, kuongeza uwazi katika utendaji, na kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili wanachama katika shughuli zao za uzalishaji na masoko.
Kupitia majadiliano ya wazi, bodi imepokea hoja mbalimbali na kuahidi kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na uongozi wa vyama husika na wadau wengine ili kuboresha huduma na kuendeleza sekta ya ushirika kwa manufaa ya wakulima wote.








