You are currently viewing SEMINA YA MAFUNZO KWA MAKATIBU MENEJA NA WATUNZA STOO WA AMCOS

SEMINA YA MAFUNZO KWA MAKATIBU MENEJA NA WATUNZA STOO WA AMCOS

Chama Kikuu cha Ushirika Milambo kiliandaa semina ya mafunzo ya siku mbili kwa Makatibu Meneja wa AMCOS na Watunza Stoo, iliyofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 10 katika Ukumbi wa ADC, Wilaya ya Urambo.

Semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo washiriki katika maeneo muhimu ya uendeshaji wa vyama vya ushirika na uzalishaji wa zao la tumbaku, yakiwemo:

  • Uandaaji wa makisio (budgeting) kwa ufanisi na kwa kuzingatia miongozo ya ushirika
  • Mbinu bora za uzalishaji wa zao la tumbaku ili kuongeza tija na ubora wa mazao
  • Masoko ya tumbaku na uelewa wa mifumo ya soko na bei
  • Usimamizi wa pembejeo kuanzia upokeaji, uhifadhi hadi ugawaji kwa wanachama
  • Matumizi ya Mfumo wa MUVU katika uandaaji wa makisio, ili kuongeza uwazi, usahihi na ufanisi wa taarifa za kifedha

Mafunzo yalifunguliwa rasmi na Mgeni Rasmi, Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Tabora, ambaye aliwapongeza waandaaji kwa kuandaa mafunzo yenye tija na kuwasisitiza viongozi wa AMCOS kutumia maarifa waliyopata kuboresha utendaji wa vyama vyao, kuimarisha uwajibikaji na kuongeza thamani kwa wakulima.

Washiriki walipata fursa ya kujadiliana, kuuliza maswali na kubadilishana uzoefu juu ya changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, hususan katika masuala ya makisio, usimamizi wa pembejeo na matumizi ya mifumo ya kidijitali.

Chama Kikuu cha Ushirika Milambo kinaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuimarisha uwezo wa rasilimali watu ndani ya vyama vya ushirika, kwa lengo la kuongeza ufanisi, uwazi na maendeleo endelevu kwa wanachama na sekta ya tumbaku kwa ujumla.

Leave a Reply